Wakati wa ukame, malisho huwa ni changamoto kubwa linalowakabili wafugaji katika ufugaji wa wa mifugo yao. Hii hupunguza ubora wa bidhaa za mifugo na vile vile huathiri uzalishaji.
Chakula cha ya mifugo kutoka kwenye vichaka asili ni fursa kubwa kwa wakulima wanapopata malisho kutoka vichakani huku wakidhibiti ukuaji wa vichaka shambani mwao. Chakula cha mifugo kutoka vichakani hutumika sana hasa katika wakati wa ukame kama chakula cha dharura na kama chakula cha ziada.
Uzalishaji wa malisho
Kwanza, kichaka huvunwa kikiwa kibichi, na huvunwa pamoja na maua, majani na mbegu zake kwa kutumia panga. Matawi membamba hutumika kutengeneza malisho bora. Baada ya kuvuna, matawi na machipukizi husagwa kuwa nyuzinyuzi ambazo huchanganywa na virutubisho na kisha kulishwa kwa mifugo papo hapo.
Vile vile, katika uhifadhi, nyuzinyuzi hukaushwa kabla ya kuchanganya na madini. Malisho ya vichakani ni suluhuhisho katika kipindi cha kiangazi au ukame, na pia ni biashara nzuri.
Uzalishaji wa malisho ya vichakani hupunguza utegemezi wa malisho kutoka nje na kwa muda mrefu, huchangia katika urejeshaji wa nyanda za malisho.