»Ufugaji wa samaki nchini Botswana«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=Bdv2HI72zgg

Muda: 

00:04:33
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Botswana Insight

Mchakato wa kukuza samaki unahitaji mbinu maalum. Hata hivyo, samaki hufugwa kwa kutumia mbinu tofauti.

Ufugaji wa samaki unahusisha kushughulikia na kukuza samaki kwenye matangi na vizimba ili kutoa chakula kwa watu. Aina za samaki zinazotumika ni pamoja na; tilapia, cat fish na aina nyinginezo. Nyavu hujengwa pande zote na chini ya kila tanki. Samaki dume huvutia samaki jike kwenye kiota chake ili kutaga mayai ambayo dume hurutubisha.

Kukuza samaki

Mayai huvunwa kwa kutumia nyavu na kisha kuhamishiwa eneo maalum ili kuanguliwa kuwa samaki wachanga. Maji huongezwa kwenye eneo la kuangulia mayai ili kuandaa hali iliyo sawa na ile ya mfumo wa mto ambayo inahitajika kwa kuanguliwa.

Samaki wachanga huchukuliwa kwenye matangi baada ya wiki sita, ambapo huhifadhiwa kwa muda wa miezi 2. Uwiano wa malisho ambayo hutolewa kwa samaki hulinganishwa na ukuaji wa samaki, yaani samaki hulishwa kulingana na uwiano wa uzito wa mwili wake.

Samaki hulishwa mara 3 kwa siku na ubora wa maji hupimwa kila siku mara 3 ili kuepuka vikwazo kwenye mfumo.

Mara samaki wanapokuwa wakubwa, basi huchukuliwa kwenye tanki maalum hadi wawe tayari kuvunwa. Samaki huvunwa kati ya miezi 6 hadi 8 wakiwa wamefikisha uzito wa 300–350g.

Samaki huchukuliwa na kupimwa kila baada ya wiki 2 na kila tanki la kukuzia samaki huwekwa alama ya tarehe ya samaki kuzaliwa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:44Ufugaji wa samaki unahusisha kushughulikia na kukuza samaki kwenye matangi na vizimba ili kuto chakula kwa watu.
00:4500:53Aina za samaki zinazotumika ni pamoja na; tilapia, cat fish na aina nyinginezo.
00:5401:20Nyavu hujengwa pande zote na chini ya kila tanki.
01:2101:30Samaki dume huvutia samaki jike kwenye kiota chake ili kutaga mayai ambayo dume hurutubisha
01:3102:24Mayai huvunwa kwa kutumia nyavu na kisha kuhamishiwa eneo maalum ili kuanguliwa kuwa samaki wachanga.
02:2502:37Maji huongezwa kwenye eneo la kuangulia mayai ili kuandaa hali iliyo sawa na ile ya mfumo wa mto
02:3802:47Samaki wachanga huchukuliwa kwenye matangi baada ya wiki sita
02:4803:06samaki wachanga huhifadhiwa kwenye matangi haya kwa muda wa miezi 2
03:0703:28Samaki hulishwa kulingana na uwiano wa uzito wa mwili wake
03:2903:37Samaki hulishwa mara 3 kwa siku na ubora wa maji hupimwa kila siku mara 3
03:3803:47Hali joto ya maji hupimwa kila siku mara 3
03:4803:56Mara samaki wanapokuwa wakubwa, basi huchukuliwa kwenye tanki maalum hadi wawe tayari kuvunwa.
03:5704:21Samaki huvunwa kati ya miezi 6 hadi 8 wakiwa wamefikisha uzito wa 300–350g.
04:2204:25Tanki la kukuzia samaki huwekwa alama ya tarehe ya samaki kuzaliwa
04:2604:30Samaki hupimwa kila baada ya wiki 2
04:3104:33Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *