Magonjwa ni moja wapo ya changamoto kuu zinazowakabili wafugaji wa kuku, na mafua ni moja wapo ya magonjwa makubwa.
Mafua ni ugonjwa wa kuku unaoambukizwa sana ambao husababishwa na bakteria na huenea sana. Maambukizo hupitia machoni na ugonjwa huo huchukua siku 1 hadi 3 kuonyesha dalili, ugonjwa huanza kuenea ndani ya siku 2 hadi 3 na kundi zima kuathiriwa ndani ya siku 10. Ugonjwa huo huenezwa kwa kugusana moja kwa moja kati ya ndege walioambukizwa na wale ambao hawajaambukizwa, na pia kupitia watu ambao hugusa ndege walioambukizwa na kisha kugusa mayai ambayo yametoka kuanguliwa au vifaranga wapya.
Dalili za ugonjwa na udhibiti
Dalili za ugonjwa za kawaida ni uvimbe usoni, uvimbe wa shavu la kuku, kupiga chafya, upungufu katika uzalishaji wa mayai, na kukosa hamu ya kula.
Udhibiti wa ugonjwa ni kwa njia ya chanjo, kutekeleza hatua bora za kuzuia magonjwa na kutenga ndege wagonjwa. Unaweza pia kutibu ndege kwa kutumia dawa kama vile; streptomycin, sulphur, sulfonamides, tylosin na dawa za erythromycin.
Ikiwa ugonjwa umenea sana kwenye shamba, ondoa na kutenga ndege walioambukizwa.
Upasuaji wa macho
Upasuaji mdogo wa jicho unaweza kufanywa ili kutibu ndege. Huku kunafanywa kwa kubonyeza jicho kwa upole, nyenzo nyeupe zinazoonekana kama usaha hutoka. Shika mdomo wa ndege na uondoe kwa upole ushaha mweupe kutoka kwa jicho. Angalia sehemu ya ndani ya jicho ili kuhakikisha kuwa hakuna mabaki yoyote.
Tumia spiriti na pamba safi kusafisha jicho. Weka dawa ya tetracycline ndani ya jicho kwa muda wa siku 5 na mpe kuku viuavijasumu.