Kwa vile maji ni kipengele muhimu zaidi katika ukuzaji wa mazao, umwagiliaji ni jambo kuu katika uzalishaji wa mazao.
Unapojenga tangi la kuhifadhia maji, zungushia eneo uzio na uboreshe miunganisho ya barabara. Kisha ondoa udongo wa juu na kuuhifadhi mahali ambapo utatumika kwa kutengeneza ardhi.
Mchakato wa ujenzi
Wakati wa ujenzi, mashine hutumika kuchimba shimo kwa kina kinachohitajika, na msingi wa tangi hutengenezwa kwa zege ambayo huimarishwa na msingi wa bamba na mbao. Kuta za tangi huimarishwa, na mchakato huo huo hutumiwa kujenga paa.
Vile vile, bomba huunganishwa kwenye tangi na mifereji ya maji hutengenezwa karibu na msingi wa tangi. Kisha tangi hujazwa na maji ambayo huachwa ndani kwa muda wa wiki moja huku viwango vya maji vikikaguliwa. Kuta za nje hufunikwa na utando ambao huzuia maji kupenya. Eneo hujazwa tena na udongo amabo hushinikizwa vizuri, kIsha paa la tangi pia hufunikwa na utando zaidi.
Sehemu iliyokaribu na tangi huinuliwa kufikia kiwango hicho hicho cha tangi. Tangi husafishwa na kuwekewa dawa za kuua viini. Vibanda vya kuuzia maji na ufikiaji wa magari pia hujengwa. Kisha uzio huzungushwa eneo na miti hupandwa kama inavyotakiwa.
Zaidi ya hayo, maduka, maofisi na kiwanja huondolewa na hatimaye udongo wa juu hurejeshwa na eneo lote hupandwa kwa nyasi.