»Uozo na ukungu mweupe kwenye njugu«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/root-and-stem-rot-groundnut

Muda: 

00:13:10
Imetengenezwa ndani: 
2019

Imetayarishwa na: 

MSSRF

Ugonjwa wa uozo (kuoza mizizi) na ukungu mweupe (kuoza mashina) huathiri sana njugu, na kupunguza mavuno. Ukungu mweupe huenezwa kupitia hewa, na maji ya umwagiliaji. Lakini maji yaliyotuama hueneza magonjwa yote mawili.

Utambuzi wa mapema, udhibiti sahihi na hatua sahihi za uzuiaji husababisha mavuno mazuri. Njugu hupandwa sana, na hutumiwa kutengeneza mafuta ya kupikia, ni chanzo cha lishe la ng‘ombe na kuku, mbolea za kikaboni, na kuongeza rutuba ya udongo kwa kuongeza nitrojeni.

Ishara na dalili za ukungu mweupe ni: Mimea hukauka na kunyauka, na mizizi ina harufu mbaya. Ukungu mweupe hutokea siku 30 baada ya kupanda. Ugonjwa huo husababishwa na kuvu inayoishi katika udongo.

Udhibiti na uzuiaji

Kwanza, Lima udongo kwa kina ili kuleta mchanga juu ambapo jua linaweza kuua kuvu. Panda kwenye vitalu vilivyoinuliwa (15 cm juu) ili kuondoa maji ya ziada. Pili, tumia kuvu yenye faida kwa ufyonzaji wa virutubisho zaidi. Palilia mimea ili iweze kunasa jua na hewa zaidi.

Kwa kuongeza ng‘oa na kuchoma mimea iliyoathiriwa ili kuzuia kuenea kwa magonjwa. Nyunyiza dondoo au mchanganyiko wa mbangimwitu ili kuthibiti mimea dhidi ya ugonjwa. Tumia jasi la unga kudhibiti uozo. Baada ya kuvuna panda mimea tofauti ili kuzuia kuongezeka kwa kuvu kwenye udongo.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:43Njugu hukuzwa sana kwa kutoa mafuta ya kupikia, chakula cha ng‘ombe na kuku, na mbolea za kikaboni. Njugu hudumisha rutuba ya udongo kwa kuongeza nitrojeni.
00:4401:42Uozo na ukungu mweupe huenea kutoka kwa mizizi, mashina na mmea wote
01:4302:17Asili ya uozo na ukungu mweupe.
02:1802:32Ukungu mweupe huenea kupitia kwa hewa na maji ya umwagiliaji. Lakini maji yaliyotuama hueneza magonjwa yote mawili.
02:3304:19Kugundua ugonjwa
04:2004:25Udhibiti na uzuiaji.
04:2605:21Panda kwenye vitalu vilivyoinuliwa
05:2207:33Tumia kuvu yenye faidha
07:3408:05Kupalilia shamba.
08:0608:40Kung‘oa na kuchoma mimea iliyoathiriwa.
08:4109:57Nyunyiza dondoo la mbangimwitu
09:5810:26Tumia jasi la unga
10:2711:15Mzunguko wa mazao
11:1613:10Muhtasari.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *