»Usimamizi wa mitende«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/date-palm-management

Muda: 

00:06:50
Imetengenezwa ndani: 
2019

Imetayarishwa na: 

Ministry of Agriculture, Iraq

Mitende hushambuliwa sana na wadudu na magonjwa kadhaa. Waakini kupogoa, kupanda mseto na kupalilia kunaweza kusaidia kuzuia magonjwa haya na wadudu.

Kupogoa ni moja wapo ya shughuli za kimsingi, ambazo huzuia wadudu kutaga mayai kwa matawi ya mitende. Kupogoa pia hurahisisha mchakato wa kupanda mitende. Kupogoa hufanywa kwa kutumia kisu maalum wakati wa masika, ambapo mimea ina unyevu wa kutosha. Hii hurahisisha mchakato wa kupogoa.

Kupanda mseto

Kupanda mseto wa mitende na mboga maalum husaidia kuvutia maadui wa asili (wadudu) ambao hula wadudu wa mitende na mayai yao. Mabaki na takataka ya mboga inaweza kuchanganywa na udongo ili kuongeza rutuba ya udongo.

Palilia chini na karibu ya mitende ili kuondoa magugu. Magugu husababisha athari kubwa katika uzalishaji kwa kuhifadhi wadudu na magonjwa. Magugu pia kushindana na mimea kwa maji na virutubisho, na pia huongeza unyevu unaosababisha kuvu.

Kufanya hatua hizi kunaweza kuongeza uzalishaji wa mitende, ubora, ukubwa wa matunda , na kuharakisha ukomavu wa mmea. Kwa hivyo, huongeza mapato ya kiuchumi. Hatua hizi pia hupunguza matumizi ya kemikali kudhibiti wadudu.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:39Udhibiti wa unyevu husaidia kudhibiti wadudu na magonjwa kadhaa kwenye mitende.
00:4000:49Udhibiti wa unyevu ni kwa kupogoa / kukata matawi, kupanda mseto na kupalilia.
00:5002:00Kupogoa huzuia wadudu kutaga mayai kwa matawi ya mitende, na pia hurahisisha mchakato wa kupanda mitende.
02:0102:25Kupanda mseto wa mitende na mboga maalum husaidia kuvutia maadui wa asili (wadudu) ambao hula wadudu wa mitende na mayai yao
02:2603:50Mabaki na takataka ya mboga inaweza kuchanganywa na udongo ili kuboresha rutuba ya udongo.
03:5105:10Palilia chini na karibu ya mitende.
05:1105:30Kupogoa, kupanda mseto na kupalilia mara kwa mara kunaweza kuongeza uzalishaji wa mitende, ubora, ukubwa wa matunda , na kuharakisha ukomavu wa mmea.
05:3106:50Hatua hizi pia hupunguza matumizi ya kemikali kudhibiti wadudu.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *