Hiki ni kipindi muhimu ambacho mnyama hupitia mabadiliko kadhaa na ya kimwili.
Kipindi hiki katika ng‘ombe wa maziwa hudumu kuanzia wiki tatu kabla ya kuzaa hadi wiki tatu baada ya kuzaa. Kwa hiyo mbinu za usimamizi wa ng’ombe katika kipindi hicho huboresha tija ya wanyama, na hivyo huongeza kipato na usalama wa chakula.
Mbinu sahihi za usimamizi
Daima toa nafasi ya kutosha kati ya mifugo wakati wa kulisha, na makazi bora ya kupumzikia ili kupunguza mafadhaiko. Pia fugia wanyama katika makazi ya kawaida, na vile vile epuka kubadilisha makazi haya mara kwa mara.
Zaidi ya hayo, toa zizi tofauti la kuzalishia na lazima hilo lisafishwe vyema ili kuepuka magonjwa. Hata hivyo, makazi ya wanyama yasiwe ya utelezi na sakafu lazima iwe kavu.
Mpe usaidizi mnyama wakati wa kuzaa ukihitajika. Baada ya kuzaa hakikisha kwamba mnyama anakula, kunywa na kucheua ipasavyo.
Hakikisha unahifadhi mnyama katika kundi aliezoea ili kuepuka msongamano, na ushindani. Wapa wanyama viwango vya juu vya chakula cha mkusanyiko wakati wa kunyonyesha ili kudumisha afya yao.
Wakati wa kulisha wanyama, wape pia malisho yenye virutubisho ili kuboresha afya yao, na vile vile chunguza wanyama mara kwa mara.
Pia, zingatia mbinu bora za usimamizi wa wanyama katika msimu wa kibaridi na kiangazi. Pia watolee chakula kilichosawazishwa ipaswavyo, na epuka kuongeza uwiano wa chakula cha mkusanyiko kighafla. Mwisho usimdhuru mnyama.