Sungura huzaa kati ya siku 29 – 32, na huzaa watoto 5 hadi 10 kila mara. Sungura wachanga hufungua macho siku 8 – 10 baada ya kuzaliwa, na huwa wamepata uzani wa 2kg katika miezi 3–4 na hivyo ni tayari kuuzwa.
Kutunza vyema sungura wajawazito, wale waliozaa pamoja na sungura wachanga husaidia kuongeza kipato na chakula kwa wafugaji. Baadhi ya shughuli za utunzaji mzuri ni pamoja na;
Kuandaa trei ndogo zilizo na uso laini kwa mfano magunia ili kutoa joto la kutosha kwa sungura wachanga. Pia, walishe sungura kwa maliso ya Ostro calcium na nyasi zilizochipuka kwa ukuaji bora.
Utunzaji na usimamizi
Wape maji safi ya kunywa, na vyakula bora baada ya kuzaa. Hakikisha kama sungura mama amewanyonyesha watoto kwa kukagua tumbo zao. Iwapo hajawanyonyesha, mlalishe chini ili watoto waweze kunyonya mara tatu kwa siku hadi wiki moja.
Zaidi ya hayo, mlishe sungura mama lishe bora mara mbili kwa siku ili kuboresha uzalishaji wa maziwa na kuhimiza ukuaji bora wa watoto. Weka watoto kwenye sanduku iliyo na gunia na taa ya umeme katika siku za baridi kwani asilimia 15–20% hufa kutokana na baridi.
Tenganisha sungura wachanga baada ili waweze kulishwa kwa urahisi. Mpe kila sungura mchanga 1ml ya maji akiwa dhaifu. Ongeza kijiko kimoja cha unga wa vitamini katika lita 5 za maji ili kupunguza matatizo ya kupumua na kuhara.
Wape sungura maji safi na majani, na uwatenganishe kwenye vizimba tofauti kwa ukuaji bora na udhibiti wa magonjwa.