»Uzalishaji bora wa maharagwe«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://sawbo-animations.org/653

Muda: 

00:07:25
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

SAWBO™ Scientific Animations Without Borders

Maharagwe ni chanzo kizuri cha protini. Hata hivyo uzalishaji wa maharagwe umepungua sana kwa sababu ya aina duni za mbegu, pamoja na sababu zingine. Hata hivyo, mbinu bora zimeletwa ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wa maharagwe katika masoko.

Maharagwe ni chanzo cha chakula na mapato kwa wakulima wengi. Kwa hivyo, tumia mbegu zenye ubora wa hali ya juu, panda kwa safu au mistari, tumia mbolea ya kuku na mbolea ya madini pamoja na kupalilia shamba ili kupata mazao zaidi.

Kupanda kwenye safu kunaruhusu maharagwe kupata virutubisho, na maji ya kutosha na hivyo kuboresha mazao. Pia kunaokoa wakati kwani kuvuna na kudhibiti magonjwa huwa rahisi. Andaa shamba kwa kulima na kulisawazisha. Tengeneza safu zikifuata mwinamo ya ardhi ili kupunguza mmomonyoko wa udongo.

Kutengeneza safu

Tumia vijiti 2 vigumu na kamba moja ndefu. Funga kamba kwenye vijiti. Simika vijiti kwenye ardhi, kutoka upande moja wa shamba hadi wingine ili kuunda mstari ulio sawa. Chimba mtaro au mfereji kwa kina cha urefu wa cm 3–4.

Weka safu ifuatayo kwa umbali wa 50 cm kutoka kwa safu zingine, na acha nafasi ya kutosha ili kupanda msetu.

Kutumia mbolea

Weka mchanganyiko kidogo wa mbolea asili na mbolea ya madini kando ya mtaro na funika mbolea kwa udongo mwembamba.

Panda mbegu kwa muachano wa angalau 10cm hadi 15 cm kutegemea na ukubwa wa mbegu.

Palilia shamba mara 3 kwa muda wa kila wiki 2 baada ya kupanda.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:27Maharagwe ni chanzo kizuri cha chakula na mapato kwa wakulima.
00:2800:54Ili kupata mazao zaidi, tumia mbegu zenye ubora wa hali ya juu, panda kwa safu.
00:5501:19Tumia mbegu zilizothibitishwa
01:2001:41Kupanda kwenye safu kunaruhusu maharagwe kupata virutubisho, mwangaza wa jua na maji ya kutosha pamoja na kuokoa wakati
01:0001:53Andaa shamba, na kutengeneza safu
01:5404:03Tumia vijiti 2 vigumu na kamba moja ndefu kuandaa safu
04:0404:46Weka mchanganyiko kidogo wa mbolea asili na mbolea ya madini shambani
04:4705:32Panda mbegu kwa muachano wa angalau 10cm na uzifunike. Palilia shamba.
05:3307:25Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *