»Video ya Mafunzo ya kukuza Pilipili«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=0uqg-wWDzdk&t=19s

Muda: 

00:12:52
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Ghana E-Agriculture

Ili kuongeza mavuno na kupanua mapato, kupanga ni muhimu. Kabla ya kupanda, wakulima wanapaswa kuzingatia ni soko ipi wanatarajia kuuzia. Soko linaweza kuwa la ndani au la kimataifa.

Pilipili hukua vyema kwenye udongo tifutifu ulio na mboji ya kutosha, usio na maji mengi, na udongo ulio na mteremko mdogo pamoja na pH kati ya 5.0 hadi 5.7. Pilipili huhitaji hali ya jua, hali ya ukame, na mvua ya kila mwaka kati ya 600 mm hadi 1250 mm. Joto bora linalohitajika ni digrii 18 hadi 32.

Mbinu za kilimo

Kuza miche kwa kupanda mbegu moja kwa kila seli ya trei au kwa kutawanya mbegu kwenye kitalu na kisha funika na safu ya 1cm ya udongo. Funika kitalu kwa matandazo hadi miche itakapoota. Funika miche na chandarua. Mwagilia maji mara kwa mara baada ya miche kuibuka.

Safisha ardhi kwa kukata miti, nyasi na na kuondoa mizizi. Lima ardhi an ongeza samadi iliyooza vizuri kwa kiwango cha kilo 3 hadi 10 kwa kila mita mraba, wiki 3 hadi 6 kabla ya kupanda.

Pandikiza miche baada ya majani 5 kuibuka, asubuhi au jioni wakati halijoto ni baridi. Udongo unapaswa kuwa laini, acha umbali sahahi kati ya mimea kutegemea aina. Wakati wa kupandikiza, mwagilia miche kwa mchanganyiko wa 5g/l NPK au 3g/l DAP. Wiki 2 kabla ya kupandikiza miche, weka mchanganyiko wa 3g NPK na 3 g salfati ya ammoniamu, na weka kando ya mimea 3g ya nitrati ya potasiamu wakati wa kutoa maua mara kwa mara kila baada ya wiki 2, na kalsiamu ya foliar iliyokithiri boroni. Baada ya kila mavuno, weka 3g ya nitrati ya potasiamu au salfa ya ammoniamu ili kurefusha muda wa kuvuna.

Tandaza kwa kutumia plastiki au nyasi, na shamba lazima lisiwe na magugu kwa kutumia dawa za kuulia magugu au kwa kupalilia na kungoa kwa mikono.

Pilipili huwa tayari kuvunwa wiki 6 hadi 8 baada ya kupandikizwa, na inapaswa kuvunwa ikiwa ya kijani au nyekundu kutegemea mahitaji ya soko. Mavuno hutofautiana kati ya tani 10 hadi 22 kwa hekta kulingana na aina na usimamizi.

Wadudu waharibifu ni pamoja na; vidukari, mchwa, utitiri na wadudud chawa. Magonjwa ni pamoja na; chule, ambayo hudhibitiwa kwa kutumia mbegu zisizo na viini, mzunguko wa mimea, na dawa ya kuua ukungu. Madoa ya bakteria yanayodhibitiwa kwa kufanya mzunguko wa mazao, na kunyunyizia dawa ya kuua kuvu iliyo na msingi wa shaba. Mnyauko wa bakteria unaodhibitiwa kwa kutumia mbegu zisizo na vimelea vya magonjwa, ufukizaji wa vitalu vya mbegu, kuua viini kwa mimea iliyopandwa kwenye vyombo. Ugonjwa wa ukungu unaodhibitiwa kwa kutumia aina sugu, mzunguko wa mazao na dawa za kuua ukungu

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:50Ili kuongeza mavuno na kupanua mapato, kupanga ni muhimu.
01:5102:50Kuna aina tofauti za pilipili tamu na pilipili hoho.
02:5103:10Tumia mbegu zilizoidhinishwa kutoka kwa kampuni zambegu zinazotambulika.
03:1103:49Pilipili huhitaji hali ya jua, hali ya ukame, na mvua ya kila mwaka kati ya 600 mm hadi 1250 mm. Joto bora linalohitajika ni digrii 18 hadi 32.
03:5004:30Pilipili hukua vyema kwenye udongo tifutifu ulio na mboji ya kutosha, usio na maji mengi, na udongo ulio na mteremko mdogo pamoja na pH kati ya 5.0 hadi 5.7
04:3104:55Andaa shamba, ongeza mbolea iliyoooza kabla ya kupanda.
04:5605:55Kuza miche kwa kupanda mbegu moja katika kila seli ya trei la kupandia.
05:5606:55Pandikiza miche baada ya majani 5 kuibuka
06:5607:51Wakati wa kupandikiza, mwagilia miche kwa mchanganyiko wa 5g/l NPK au 3g/l DAP. Wiki 2 kabla ya kupandikiza miche, weka mchanganyiko wa 3g NPK na 3 g salfati ya ammoniamu.
07:5208:25Baada ya kila mavuno, weka 3g ya nitrati ya potasiamu au salfa ya ammoniamu
08:2609:00Tandaza shamba kwa kutumia plastiki au nyas.
09:0109:24Mwagilia shamba wakati wa kuchana maua.
09:2510:08Palilia shamba dhidi ya magugu.
10:0910:55Pilipili huwa tayari kuvunwa wiki 6 hadi 8 baada ya kupandikizwa.
10:5612:52Dhibiti wadudu na magonjwa.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *