Ng‘ombe aina ya friesian hutoa maziwa mengi, wanaweza kutoa lita 110 za maziwa kwa siku. Wakati wa kuzaliana tafuta ng‘ombe dume na jike ambao watazaa ndama anayetoa maziwa mengi.
Malisho yanahitaji kuwa na madini na nishati. Changanya nyasi ya napier, bracharia, desmodium, lucena na unga wa maziwa kwa uzalishaji bora wa maziwa.
Usimamizi wa ng‘ombe
Ng’ombe hawapaswi kulala kwenye sehemu yenye unyevu na matope ili kuzuia wadudu na magonjwa. Safisha banda la ng’ombe.
Uzalishaji wa maziwa husaidia kuboresha maisha ya watu. Ng‘ombe pia huzalisha mbolea ambayo inaweza kutumika kama chanzo cha mapato.
Ng‘ombe wanaweza kukamuliwa asubuhi na mchana kila siku.
Taasisi za mafunzo
Tembelea taasisi za mafunzo ili kujifunza jinsi ya kutunza mifugo. Usitumie mbinu za zamani za ufugaji.
Taasisi ya mafunzo zinafaa kuleta taarifa kwa wakulima. Kwa kumueleza mkulima juu ya mabadiliko ya teknolojia, kuwaelimisha vijana juu ya umuhimu wa kufuga na kuangalia miradi yenye manufaa kwa wafugaji.
Taasisi za mafunzo zinapaswa kuwaelimisha wakulima juu ya kuboresha uzalishaji, msimu bora wa upandaji na uongezaji thamani. Mabwawa husaidia kuhifadhi maji na yanaweza kutumika kumwagilia mimea wakati wa kiangazi.