Vichaka vinaweza kuwa changamoto shambani au msituni kwa sababu huathiri ukuaji wa mazao na miti.
Kuna njia tofauti za kudhibiti magugu na vichaka. Wakati shina za vichaka ni ndogo, unaweza kuvidhibiti kwa ufanisi na dawa ya kuua magugu, lakini wakati shina linakuwa kubwa, basi unahitaji kutumia matibabu halisi ya kuingiza viuatilifu kwenye gome la mti.
Vichaka vya shina kubwa
Matibabu ya ya kuingiza viuatilifu kwenye gome la mti yana ufanisi mzuri kwenye vichaka virefu na vile vyenye mashina makubwa.
Ili kuua magugu kwa mbinu ya kuingiza viuatilifu kwenye gome, hakikisha kuwa una viuatilifu vinayopendekezwa, kinyunyizio cha dawa kinachoweza kurekebishwa na mafuta maalum ambayo husaidia kemikali kupenya shina.
Pia hakikisha kuwa una vifaa vya kujikinga na hivi ni pamoja na miwani , glavu, shati la mikono mirefu, suruali ndefu, viatu vigumu.
Mazingatio
Kabla ya kutumia dawa hiyo, sio tu ukubwa wa shina ambao ni muhimu lakini pia maumbile ya gome la mti.
Njia bora ya kuamua ikiwa kama utumiaji wa viuatilifu utakuwa na ufanisi ni kukwaruza gome la shina la mti kwa kucha na ikiwa unaweza kuona rangi ya kijani kibichi basi inaonyesha kuwa dawa ina ufanisi mzuri.
Nyunyiza dawa kwa kutumia kinyunyizio kinachoweza kurekebishwa huku ukitumia shinikizo la chini. Hakikisha unanyunyizia kila shina hadi inchi 12 -20 kutoka ardhini.
Hakikisha unatumia viuatilifu vinavyoyeyushwa kwenye mafuta kwa sababu viuatilifu vinavyoyeyushwa kwenye maji vinaweza kuoshwa mvua, na hivyo kuvifanya kuwa na ufanisi mdogo.