Nyanya ni mojawapo ya mazao ambayo ni rahisi kupanda kwa sababu mmea unapoanza kuota, mbolea na dawa za kuua wadudu huwekwa.
Kabla ya kupanda kukumbuka kuweka mbolea na kwa kuzichanganya na unga wa humi ambao husaidia katika ufyonzaji wa virutubisho. Ingawa kilimo cha nyanya kina changamoto kadhaa kama vile wadudu na magonjwa; kinapendelewa na wakulima kwa kuwa ni chanzo cha kipato, na pia hakihitaji kazi nyingi.
Kushughulikia nyanya
Nyunyiza mimea ya nyanya hadi itakapoanza kutoa matunda. Hii ni kwa sababu mmea unapoanza kutoa matunda huhitaji maji zaidi. Pogoa mmea ili kuondoa majani mazee, majani yaliyo na ugonjwa n.k kila wiki.
Ondoa machipukizi yanayoota kati ya matawi mawili kwa vile hayatatoa matunda, bali hushindania virutubishi. Simika vijiti ili kuimarisha mimea ya nyanya baada ya kupandikiza, na hivyo kuepuka uharibifu wa shina.
Muda wa ukomavu
Matunda ya nyanya kawaida huachwa kukua hadi kugeuka kutoka rangi ya kijani hadi dhahabu. Huu ndio wakati sahihi wao kuvunia.
Mmea huanza kuchanua maua wakati unakaribia mwezi mmoja na nusu. Katika miezi miwili, mmea huanza kutoa matunda, na hivyo mbolea huongezwa baada ya kila mwezi.
Inachukua muda wa miezi mitatu kwa matunda ya kwanza kuwa tayari kuvunwa.
Udhibiti wa wadudu
Wadudu na magonjwa kama vile kantangaze huathiri majani ya mmea, na ni changamoto kwa kilimo cha nyanya. Kunyunyizia dawa za wadudu husaidia kudhibiti.
Ugonjwa wa bakajani katika nyanya ni tatizo lingine na linaweza kudhibitiwa kwa kunyunyizia viuawadudu katika wiki ya kwanza, na viuakuvu katika wiki ya pili.