Ufugaji wa nyuki husaidia kuongeza kipato. Ili kuongeza uzalishaji wa asali wafugaji lazima wahakikishe ukaguzi wa mizinga pamoja na uvunaji sahihi wa asali ili kupata bidhaa bora.
Kuna dalili zinazosaidia wakulima kutambua makundi ya nyuki yaliyo tayari kuvunwa, miongoni mwao ni pamoja na, mimea kudondosha maua na majani, kukomaa kwa matunda, kukomaa kwa mazao mengine ya shambani, kifo cha nyuki dume kwenye kundi, kupungua kwa sauti ya nyuki kwenye mzinga, mizinga kuwa mizito. Ukaguzi wa mara kwa mara wa mizinga husaidia kufuatilia hali ya mizinga, kuangalia uvamizi wa wadudu na kutambua makundi yaliyo tayari kuvunwa.
Mambo yanayohimiza uzalishaji wa asali
Chanzo cha chakula; uwepo wa mimea yenye maua karibu na mzinga husababisha uzalishaji zaidi wa asali.
Ukubwa wa kundi; kadiri kundi linavyokuwa dogo ndivyo asali inavyozalishwa kidogo, na kadiri kundi linavyokuwa kubwa ndivyo asali inavyozalishwa zaidi.
Uchanuaji wa maua katika eneo; mimea inayochanua maua mwaka mzima huongeza uzalishaji wa asali kuliko ile inayochanua maua miezi 3–4 kwa mwaka.
Uwezo wa nyuki kuhifadhi asali; nyuki wenye uwezo wa kuhifadhi asali huongeza kiwango cha uzalishaji kuliko wale ambao hawawezi kuhifadhi asali.
Hatua za kuvuna asali
Anza kwa kutafuta mshirika wa kuvuna naye, na kuvaa nguo ndefu na tumia kitoa moshi ili kujikinga dhidi ya nyuki.
Kisha tayarisha moshi bila kutumia plastiki wala majana yenye sumu kwani hizi zinaweza kushusha ubora wa asali.
Funika mizinga ya nyuki polepole, epuka kuvuna masega yenye mabuu ili kuepuka kuvuna mabuu ambayo yanaweza kukua na kuwa nyuki.
Uvunaji ufanyike kwa masega yaliyojazwa robo tatu, na usivune asali yote kutoka kwenye mzinga ili kuzuia kundi la nyuki kuhama.