Mpunga ni ambalo kwa ujumla hukua katika maeneo yenye maji mengi na huhitaji joto la nyuzi 20 – 30 na ardhi tambarare. Mpunga wa nyanda za juu hauhitaji kusawazisha kitope wakati wa kuandaa ardhi.
Mpunga wa nyanda za juu hukomaa haraka na unahitaji maandalizi kidogo ya ardhi kuliko aina ya mpunga wa nyanda za chini. Hata hivyo, ni bora kupanda mpunga kwenye udongo mzito wa mfinyanzi kwa sababu ya hitaji lake la juu la maji, na pia udongo wa mfinyanzi una uwezo mkubwa wa kuhifadhi maji. Hatua tofauti za ukuaji wa mpunga huhitaji kiwango tofuati cha maji. Hatua ya mpunga mchanga huhitaji maji ya kutosha tu kwa ukuaji wa kawaida, lakini maji zaidi yanahitajika katika hatua ya kilele. Kwa maeneo yenye mvua ya kutosha tumia aina ya mpunga wa nyanda za juu.
Mbinu bora za usimamizi
Kwanza fyeka na safisha ardhi, tengeneza kingamaji ambazo hutumika kuhifadhi maji. Kisha lima, lainisha na sawazisha udongo ili kupunguza upenyezaji wa kina wa maji, kurahisisha kupandikiza, kupunguza ukuaji wa magugu na kuingiza hewa ya oksijeni kwenye udongo wa juu.
Zaidi ya hayo dhibiti magonjwa makuuu kama vile ukungu, madoa ya kahawia na kubadilika rangi. Tumia aina sugu, mbinu bora za kiasili za kilimo ili kudhibiti kutu za majani , punguza matumizi ya nitrojeni ambayo ina potasiamu kidogo ili kupunguza matukio ya ukungu, tumia mbegu safi zenye afya ambazo zimetibiwa kudhibiti mbegu vimelea vya magonjwa. Nyunyizia dawa za kemikali ili kudhibiti magonjwa ya ukungu.
Mwishowe, iwapo vibarua ni ghali, tumia njia ya upandaji ya kutawanya mbegu japo kuwa inapunguza uotaji. Kinyume na hapo, iwapo vibarua ni nafuu, pandikiza kwa umbali wa sm 30 x 30 ili kuzuia ukuaji wa magugu.