Mbinu ya kilimo cha bustani za nyumbani inalenga kuzalisha mboga na matunda zaidi, ili kukidhi mahitaji ya chakula nchini Kenya, huku ikitumia nafasi ndogo za nyumbani.
Bustani ndogo huruhusu familia zilizo hatarini kukidhi mahitaji yao ya vitamini, madini na protini kwa kuzitoa ufikiaji wa moja kwa moja kwa mboga zenye lishe kila siku. Pia hutoa chanzo cha mapato ya ziada kutokana na mauzo ya mboga zilizobaki.
Bustani ndogo
Kilimo cha bustani ndogo kinaelezewa kama kilimo kinachohusisha ukuzaji wa mazao katika vyombo kwenye nafasi ndogo. Aina tofauti za vyombo ambavyo vinaweza kutumika kama vile chupa za plastiki, mikebe ya takataka. Kulima bustani kunahitaji juhudi kidogo za kimwili.
Mahitaji ni pamoja na : chupa, miche, waya wa kufunga au uzi, mkasi, samadi, udongo, maji, misumari, koleo na mbao ili kutengeneza muundo uliosimama.
Utengenezaji
Tambua eneo lako ili kuunda bustani yako. Katika mijini, uani mwa nyumba yako au barazani ni bora kwa muundo.
Kata waya ya kufungia ya cm 120 na kuiweka kwenye mashimo yaliyo kwenye chupa. Acha umbali wa cm 30 kati ya chupa. Tumia uzi kuzininginiza kwenye ufito. Jaza chupa na udongo uliochanganywa na mbolea kwa uwiano wa 1: 1. Mwagilia maji, na kisha tengeneza mashimo ya nkupandia kwenye udongo, na panda letasi, mboga na viungo.