Karoti huathiriwa sana na joto kali. Hata hivyo, halijoto iliyo chini ya nyuzi joto 10 husababisha karoti ndefu nyembamba.
Karoti zinapaswa kuhifadhiwa kwenye makreti mahali panapopitisha hewa ili kuepuka uozo na ukungu. Kwa mavuno mengi, karoti huhitaji udongo wenye rutuba, usio na tindikali, ambao pia hautuamishi maji. Mashamba ya karoti yanapaswa kuwekwa katika maeneo yenye mwanga wa jua kamili, na vile vile kivuli kidogo na halijoto bora iliyo kati ya nyuzi joto 16-24 Celsius. Kuna mahitaji mbalimbali yanayohitajika ili kuanzisha shamba la karoti, miongoni mwa haya ni pamoja; na ardhi, mbegu, na mbolea.
Kupanda karoti
Andaa ardhi vizuri na panda mbegu zilizoidhinishwa kwa kina cha 6mm na muachano wa 5cm kutoka kwa kila mmea. Kisha funika mbegu na safu nyembamba ya udongo, waweza pia kupanda mbegu kwa kutawanya. Hata hivyo, huku hufanya udhibiti wa magugu kuwa mgumu sana. Weka matandazo kwenye mashamba ya karoti ili kuhifadhi unyevu wa udongo, ongeza mboji iliyooza kabla ya kupanda.
Usimamizi na uvunaji
Mwagilia mazao asubuhi na jioni pamoja na kuweka matandazo ili kuhifadhi unyevu wa udongo. Pia weka mboji iliyooza na kuifunika na majani ya mnazi ili kuhifadhi unyevu wa udongo, pia epuka jua la moja kwa moja kufijia miche. Mwagilia miche kwa uangalifu na uondoe mabonde ya udongo yaliyogandamana ili kuhimiza uotaji wa mbegu. Hatimaye, vuna miezi 2-3 baada ya kupanda, wakati mizizi ina kipenyo cha 3cm.
Magonjwa na wadudu
Vidukari hupatikana chini ya majani, husababisha kudumaa na umanjano wa majani. Vidukari wanaweza kudhibitiwa kwa kutumia mbegu zinazostahimili wadudu pamoja na viuawadudu. Viwavi hudhibitiwa kwa kuondoa uchafu shambani na kufanya mzunguko wa mazao. Bakajani husababisha umanjano kwenye majani na hudhibitiwa na dawa za ukungu. Kuoza kwa mizizi hutokana na matumizi mengi ya mboji. Mwishowe, ubwiri unga hudhibitiwa na kuacha nafasi sahihi kati ya mimea pamoja na kufanya mzunguko wa mazao.