Kujifunza hatua bora za kuvuna na kuelewa mda maalum ni njia nzuri ya mkulima kufuata ili afanikiwe nakupata mavuno.
Mahindi huvunwa yakiwa yamekomaaa kabisa, na hapo maganda yaanza kukauka na kubadilika kwa rangi ya manjano. Kisha, ndevu za hindi huanza kudondoka . Unaweza kukagua ugumu wa hindi kwa kufinya punje zake kwa vidole. Basi mahindi yamekomaa kabisa ikiwa hakuna mikwaruzo inaoachwa baada ya kufinya. Ukiona ishaara hizo, basi usichelewe kuvuna, lasivyo mahindi yako yatavamiwa na wadudu.
Hatua za Kuvuna.
Kabla ya kuvuna mahindi, lazima ujiandae na kusafisha eneo la kuhifadhi. Pia, zana za kuvunia kama vile beseni ziwe safi na kavu. Tafuta watu wa kukusaidi katika hatua za kuvuna.
Mahindi yakiwa yamekomaa, basi endelea na kuvuna. Endapo umepanda aina mbalimbali za mahindi, endelea na kuvuna aina za kisasa. Baada yapo, vuna aina za kienyeji kwa sababu yanaweza kustahimili uvamizi wa wadudu.
Unafaa kuondolea maganda shambani ili usilete nyumbani maganda yalio vamiwa na wadudu. Ukiwa nyumbani, basi tenganisha mahindi ili kuhakikisha kwamba mahindi yanaohifadhiwa ni mazuri. Choma mahindi yalioharibiwa na kuvu.