Soya ni zao la kunde ambalo hukomaa ndani ya wiki 14 hadi 16. Uvunaji na uhifadhi sahihi, huongeza ubora wa nafaka na hupunguza hasara baada ya mavuno.
Hata hivyo vuna asubuhi mapema, linda maharagwe ya soya dhidi ya mvua na wanyama na uache mabaki shambani bila kuchoma kwani haya yanaweza kutumika kama chakula cha mifugo na kuongeza mboji na virutubisho kwenye udongo.
Kuvuna na kuhifadhi
Vuna wakati maganda ya mbegu yamekomaa na yamegeuka rangi ya hudhurungi au wakati mbegu zinapotoa sauti zinapotikiswa.
Linda soya dhidi ya mvua, wanyama na juu ya ardhi wakati unapokausha, ili kuongeza ubora wa nafaka na kupata bei ya juu.
Pura kwa uangalifu ili kuepuka kuharibu nafaka na kisha, kukaushia kwenye eneo safi.
Pepeta, ondoa nafaka zilizovunjika, na aina zingine za nafaka, kisha kausha kwa siku 3.
Weka nafaka kwenye mifuko safi iliyokaushwa, kisha weka kwenye chumba safi cha kuhifadhia, juu ya ardhi ili kudhibiti magonjwa na wadudu.
Safisha chumba cha kuhifadhia, weka nafaka juu ya ardhi na bila mgusano na ukuta ili kuzuia ukungu.
Kagua ili kuondoa nafaka zilizoshambuliwa na mbovu ili kudhibiti kushusha ubora wa nafaka nyingine.